NJE YA BOX

“Vijana tujenge uthubutu”- Ibrahimu Juma

Posted on

“Kama ukiendelea kukaa vijiweni na kupiga kelele juu ya tatizo la umasikini linalokukabili basi utabaki kuwa mpiga filimbi tu na kamwe hautatoka. Msikilize IBRAHIMU JUMA kijana mwenye fikra kubwa na maono chanya akitoa maarifa kwa vijana wa kitanzania jinsi ya kuondokana na umasikini ndani ya kipindi cha NJE YA BOX

NJE YA BOX

“Kila Mtu anaweza kuwa Tajiri” – Dominic Haule

Posted on

Nje ya Box imekutana na Bwana Dominic Haule, mjasiriamali anayeamini kuwa kika mtu anaweza kuwa tajiri. Usemi wake unatokana na imani yake kwa jamii kwamba wajasiriamali wanaweza kupambana vilivyo ili kufikia malengo, na bado nchi yetu ina rasilimali za kutosha. Pia anawaasa wafanyabishara kutokata tamaa na kutodharau fursa za kibiashara zinazojitokeza kwani utajiri unawezekana.

NJE YA BOX

Nje Ya Box na Elihabu Maganga

Posted on

Mjasiriamali Elihabu Maganga, anatuelezea umuhimu wa kuwa na ndoto kubwa, umuhimu wa kuwaza kujiajiri na kuajiri wengine kuliko kuwa na fikra mgando za kuishia kuajiriwa tu. Vijana wanatakiwa kujaribu kufanya uwekezaji wa mitaji (fedha), muda na kujiendeleza kielimu kwenye ujasiriamali.

NJE YA BOX

Nje Ya Box na Dr. Vicensia Shule (UDSM)

Posted on

Nje ya box ni segment inayohusisha wajasiriamali mbalimbali ambao hutoa ushauri na njia mbalimbali za kutatua matatizo ya wajasiriamali. Ushauri unaotolewa na Dr. Vicencia Shule kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) ambapo anagusia maswala ya kugeuza wazo kuwa biashara. Uoga wa watu kusema/kuandika mawazo yao unapelekea wajasiriamali wengi kushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea.