Biashara ya viungo vya chakula inavyowaingia pesa vijana.

Kutana na vijana wanaojihusisha na utengenezaji wa viungo vya chakula na vinywaji ambao wamejikita kwenye bisahara hii na kwa sasa wanayaona matunda yake. Vijana hawa wanakamua mafuta kutokana na maganda ya miti na matunda mbalimbali kama limao, ndimu, machaichai na machungwa. Wana mashamba makubwa katika mikoa mbalimbali Tanzania ambapo wanavuna malighafi hizi na kuzitengeneza kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *