NGOWI TV NI NINI?

NGOWI TV ni kituo cha televisheni katika mtandao kinachojikita katika kutoa elimu na habari zilizochambuliwa kuhusu masuala ya uchumi, biashara na maendeleo duniani na Tanzania. Inafanya chambuzi za kisayansi za mambo ya uchumi na biashara na jinsi mambo haya yanahusiana na maendeleo katika ujumla wake. Inalenga kuwa kituo mahiri (centre of excellency) katika kuelimisha, kuarifu na kushauri jamii na wafanya maamuzi kuhusu uchumi, biashara na maendeleo katika mapana yake.

SIFA ZA MJASIRIAMALI MZURI

Huu ni mfululizo wa wa vipindi vya kijasiriamali vya Prof: Ngowi vinavyolenga kutoa elimu ya masala ya kijasiriamali kwa watanzania wote ili kuwawezesha upata maarifa na hatimaye maarifa nayo yawe msaada kwao binafsi na Taifa kwa ujumla. Jina la kipindi ambalo pia ndilo jina la somo ni SIFA ZA MJASIRIAMALI BORA/MZURI. Kipindi hiki imegawanywa katika sehemu kuu tatu ili kukuwewezesha wewe mtazamaji kukipata na kujifunza kwa urahisi. ukifuatilia vipindi hivi kwa ufasaha, hakika hautabaki jinsi ulivyo.

NJE YA BOX

Nje ya box ni segment inayohusisha wajasiriamali mbalimbali ambao hutoa ushauri na njia mbalimbali za kutatua matatizo ya wajasiriamali. Ushauri unaotolewa na Dr. Vicencia Shule kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) ambapo anagusia maswala ya kugeuza wazo kuwa biashara. Uoga wa watu kusema/kuandika mawazo yao unapelekea wajasiriamali wengi kushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea.